DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 28,2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi,Zuhura Yunus.
Balozi Siwa ameapishwa Agosti 28, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bw. Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Balozi Siwa ameapishwa Agosti 28, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bw. Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.