Rais Dkt.Samia awataka wakulima kujiwekea akiba

MBEYA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha na kuuza ziada kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili wapate faida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere aliyeikabidhi kwa niaba ya Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane.(Picha na Ikulu).

Rais Samia ametoa wito huo leo kwenye kilele cha maonesho ya kilimo na maadhimisho ya sherehe za Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imedhamiria kuwa na uwezo wa kuhifadhi chakula tani 3,000,000 ifikapo mwaka 2030 ili ziweze kusaidia nyakati za dharura.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema serikali inaendelea kufanya jitihada za makusudi za kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo kwa kuwa kundi hilo ndilo nguzo muhimu kwa uchumi wa taifa.

Rais Samia pia amesema jitihada hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa Programu ya miaka 8 inayoitwa Building a Better Tomorrow ( BBT) ambapo vijana 812 (wanawake 282 na wanaume 530) wanaendela na awamu ya kwanza ya mafunzo ya kilimo biashara katika vituo atamizi 13.

Vile vile, Rais Samia amesema juhudi hizi zimeifanya Tanzania kutambulika kimataifa na kuchaguliwa kuwa Mwenyeji wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (African Food Systems Forum) litakalofanyika tarehe 5 -8 Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Halikadhalika, Rais Samia amesema Jukwaa hilo litaipatia Tanzania fursa za kibiashara na kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika, kwa kuwa na mifumo jumuishi ya kuimarisha kilimo, mifugo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news