Rais Dkt.Samia awataka wakuu wa mikoa kuwajibika

PWANI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kuendana na mabadiliko ya dunia.

Rais Dkt.Samia ametoa agizo hilo leo Agosti 27,2023 wakati akifunga mafunzo ya viongozi hao kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere.

Aidha, Rais Dkt.Samia amewataka viongozi hao kuwa wepesi kukabiliana na mabadiliko hayo ili kuendana na mfumo wa kidunia wa kisiasa na kiuchumi bila kusubiri maelekezo kutoka juu.

Vile vile, Rais Dkt.Samia amewataka viongozi huo kujiamini na kuwa na hoja ya kutetea maamuzi wanayoyafanya kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla kwa kuzingatia miongozo, kanuni na sheria.

Rais Dkt.Samia pia amewataka kuhakikisha usalama wa vijana kwa kusimamia miradi inayowahusisha ambayo mingi hutumika kupenyeza ajenda zinazopotosha maadili ya vijana na utamaduni wa taifa.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kuacha kupuuza wananchi hivyo wawatumikie kwa kuwahudumia na kushughulikia kero,malalamiko na mahitaji yao.

Hali kadhalika, Rais Dkt.Samia amewataka watumishi serikalini katika idara tofauti kwenye ngazi za mikoa kutumia fedha za maendeleo zinazotolewa kwa maslahi ya wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news