Rais Dkt.Samia mgeni rasmi Simba Day

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumapili ya Agosti 6,2023.
Ni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam ambao una uwezo wa kuketisha mashabiki 60,000 kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC imefafanua kuwa, Simba Day ya mwaka huu ni kubwa na maalum ndio maana wamemuomba Rais Dkt.Samia kuwa mgeni rasmi.

"Uongozi wa klabu unamshukuru Rais Dkt.Samia kukubali mwaliko wetu na kuwa miongoni mwa Watanzania 60,000 watakaohudhuria Simba Day ya mwaka 2023.

"Maandalizi ya Tamasha hili la kihistoria yanaendelea vizuri, kila kitu kipo kwenye mstari huku taratibu zikiwa vizuri ikisubiriwa siku yenyewe kufika.

"Tayari tiketi za Tamasha zimeuzwa zote hivyo ni wazi mashabiki 60,000 wamethibitishwa kuhudhuria Simba Day 2023 ikiwa ni historia mpya kwa kuwa haijawahi kutokea,"ilifafanua sehemu ya taarifa ya Simba SC..

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news