Rais wa Algeria ateta na Waziri Dkt.Tax

ALGIERS-Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Abdelmadjid Tebboune amekutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alipomtembelea Ikulu jijini Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Abdelmadjid Tebboune akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alipomtembelea Ikulu Jijini Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria unaofanyika kuanzia tarehe 30 Julai 2023 hadi 1 Agosti 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Abdelmadjid Tebboune akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mej. Jen. (Mst) Jacob Kingu ambaye alifuatana na Waziri Tax Ikulu ya Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023. 

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na kidiplomasia ili kuweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zao.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Abdelmadjid Tebboune akisalimiana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal baada ya kuwasili Ikulu Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023.

Aidha, katika kuendelea kuimarisha ushirikiano Waziri Tax pamoja na majukumu mengine, atazindua Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 2 Agosti 2023 Jijini Algiers.
Baada ya kuwasili katika Ikulu ya Algiers, Algeria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiongea mbele ya waandishi wa Habari katika Ikulu ya Algiers baada ya kumalizika kwa mazungumzo yake na Mheshimiwa Rais Abdelmadjid Tebboune Ikulu Algiers, Algeria tarehe 1 Agosti 2023.

Uzinduzi wa ubalozi huo, ni hatua muhimu hasa wakati huu ambapo viongozi hao wamekubaliana kuinua sekta za uchumi ambazo ni pamoja na biashara, uwekezaji, nishati, madini, elimu, sayansi na teknolojia, afya na utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news