DAR ES SALAAM-Ripoti ya Uthabiti wa Kifedha Tanzania Disemba 2022 imeonesha kuwa,Sekta ya Uendelezaji Milki iliendelea kuwa tulivu baada ya kupitia changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na janga la UVIKO-19.
Kiwango cha umiliki wa mali za biashara kiliongezeka, ikionesha ufufuaji wa biashara kutokana na janga hilo.Mali zilizochaguliwa za kibiashara zilikuwa na kiwango cha umilki wa zaidi ya asilimia 50.
Hivyo, kuonesha utulivu katika soko la uendelezaji milki. Baadhi umiliki wa mali za kibiashara ulibakia chini ya asilimia 50, kwani sekta hiyo bado ilikuwa haijapata nafuu kikamilifu kutokana na janga hilo, lakini pia kutokana na kuhamishia ofisi za Serikali Dodoma.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kila mwaka ambayo huwa inatolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikiwa imetayarishwa na benki hiyo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha nchini.
Bei za ukodishaji na uuzaji wa makazi ziliongezeka katika maeneo ya kawaida na ya chini. Bei ya kukodisha ya kila mwaka kwa maeneo ya Serikali jijini Dar es Salaam iliendelea kuimarika. Hali inayoakisi ufufuaji wa biashara, ukuaji wa uwekezaji, pamoja na ongezeko la mapato ya wapangaji.Bofya hapa, kupakua ripoti yote