Serikali yagusia kuhusu gharama za kusafisha figo

DAR ES SALAAM-Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa,Serikali itahakikisha gharama za usafishaji figo zinakuwa nafuu ili kuokoa maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Waziri Ummy ameyabainisha hayo wakati akitoa ufafanuzi kufuatia hoja ya mmoja wa wananchi katika mtandao wa Twitter.

Amesema, huduma za kusafisha figo kwa wengine ni biashara ya faida kubwa, lakini Serikali itahakikisha huduma hiyo ni ya gharama nafuu ili kuokoa maisha ya wengi.

“Ni sahihi kabisa gharama za kusafisha figo nchini zipo juu sana wastani wa dola za Marekani 100 (sawa na shilingi 250,000) kwa awamu moja India ni kama dola za Marekani 30 (sawa na shilingi 74,000) kwa siku.

"Ambapo hata hivyo, hata hiyo dola 30 kwa siku bado ni kubwa sana kwa watanzania wengi ambayo ni kama shilingi 600,000 kwa mwezi bado wananchi wengi hawawezi kumudu,”amefafanua Waziri Ummy.

“Serikali itaendelea kuboresha huduma za usafishaji figo na kuwekeza zaidi kwenye huduma hizi ili mwananchi aweze kumudu gharama hizo, tunawakaribisha wadau ambao wapo tayari kushirikiana nasi kufikia azma hii, tutaendelea nao,”amesisitiza Waziri Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news