Serikali yaguswa na Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Balozi Dkt. Pindi Chana amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) za kuandaa Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili Ndani na Nje ya Nchi kwa miaka 10 kuanzia 2022 hadi 2032.

Mkakati huo ulioanza utekelezaji wake mwaka 2022 umelenga kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakuwa bidhaa itakayosaidia kutatua changamoto ya ajira kwa wasomi wa Kiswahili walio ndani ya nchi.

Mhe.Chana ameagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinashiriki katika utekelezaji wa mkakati huo, kwani ni mkakati wa taifa na kila Mtanzania anapaswa kushiriki katika kuutekeleza.

Katika hatua nyingine, Mhe.Pindi Chana ameliagiza BAKITA kuhakikisha kila halmashauri nchini inapata nakalamango na nakalatepe ya Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili.

Mhe.Waziri Pindi Chana amesisitiza kuwa, mkakati huo unatekelezwa kwa asilimia mia moja kwa sababu utakuwa chachu ya ongezeko la pato la taifa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inatuimika kuvuta watalii nchini.

Waziri ameongeza kuwa kwa sasa soko la ukalimani limezidi kukua na kwa sasa Jumuia ya Afrika Mashariki inahitaji naUmoja wa Afrika wanahitaji wakalimani.

Akiwasilisha Mkakati huo, Katibu Mtendaji wa BAKITA, Bi. Consolata Mushi, amesema kuwa dira ya Mkakati wa Taifa wa Ubidhaishaji wa Kiswahili ni kuwa na mfumo madhubuti wa kitaasisi katika kuratibu, kusimamia na kukuza maendeleo ya Kiswahili kitaifa,

Kikanda na kimataifa na dhima ya mkakati huo ni Kusimamia, kuratibu na kushiriki kikamilifu katika kustawisha maendeleo na matumizi ya Kiswahili kitaifa na kimataifa.

Bi. Consolata ameeleza kuwa, mkakati huo umebainisha fursa mbalimbali za lugha ya Kiswahili ikiwamo kuuza machapisho mbalimbali ya Kiswahili ili kuinua vipaji na hali ya waandishi wazawa. Bi. Mushi amesema kuwa lengo kuu la mkakati ni kukuza Kiswahili ili kiwe chachu ya maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news