Serikali yaipa kongole DART

DAR ES SALAAM-Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amepongeza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kwa kutumia mfumo wa kudhibiti kugushi tiketi (msimbo code) na kuanza mchakato wa matumizi ya kadi maalum kwa wateja wake.
Mhandisi Mativila ametoa pongezi hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi hiyo na mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka awamu ya kwanza na ya pili katika eneo la Gerezani, pamoja na mpango mkakati wa DART wa kuanzisha eneo la kibishara mkabala na kituo hicho cha Gerezani.

Naye Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Edwin Mhede amesema, Dart ina mpango wa kuanza rasmi matumizi ya kadi mapema baada ya mwezi Machi, mwakani.

"Tayari kadi zimekwishanunuliwa na mchakato wa kufunga mfumo wa kadi unaendelea na mwezi Machi utaanza kuwekwa kwenye mageti,"amesema.

Pia, amesema DART inatarajia kuanza safari kutoka Mbagala hadi Gerezani mapema mwezi Machi, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news