KATAVI-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ameitaka Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Katavi kuainisha maeneo ya uwekezaji huku akisisitiza utangazaji wa kimkakati katika maeneo hayo ufanyike ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje nchi kuwekeza katika hifadhi hiyo.

"Ainisheni maeneo hayo kwani Wawekezaji wengi wanataka kuwekeza katika hifadhi hii," Mhe. Masanja amesisitiza.
.jpeg)
Katika hatua nyingine, Mhe.Masanja ameendelea kuwasisitiza Wananchi kuacha kuvamia maeneo ya Hifadhi huku akiwataka wahifadhi kuendelea kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa maeneo hayo kitaifa na kimataifa.

Hifadhi ya Taifa Katavi ni hifadhi ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 21 nchini ikiwa na kilomita za mraba 4,471.