DAR ES SALAAM-Kikosi cha Simba SC kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Alhamisi katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Baada ya mazoezi hayo kikosi kinajiandaa na safari ya Tanga kamili kwenda kushiriki michuano ya Ngao ya Jamii ambayo safari hii inashirikisha timu nne. Mbali na Simba na Singida Fountain Gate wengine ni Yanga SC na Azam FC zote za jijini Dar es Salaam.