DAR ES SALAAM-Tanzania imendelea kufanya vema katika michezo mbalimbali,ambapo kwa sasa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa vijana chini ya umri wa miaka 18.
Rais wa CECAFA, Wallace Karia akimkabidhi Kombe la ubingwa wa CECAFA U18 nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake U18,Noela Luhala.
Ni baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda ndani ya Uwanja wa Azam Complex uliopo Kata ya Chamazi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Winfrida Gerlad dakika ya 42 ndiye aliwapa tabasamu Watanzania kupitia bao lake la pekee ambalo limeiwezesha timu hiyo kumaliza kwa alama 12.
Ni alama ambazo ni zidio la tatu zaidi ya wageni wao kutoka nchini Uganda baada ya michezo yote minne ya michuano hiyo muhimu .
Aidha,timu tano zilishiriki michuano hiyo,huku Ethiopia ikimaliza na alama sita nafasi ya tatu, Burundi nafasi ya nne alama tatu na Zanzíbar ambayo haikuvuna chochote ikisindikiza michuano hiyo.