RUVUMA-Mhashamu Mkuu Damian Dallu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Songea ametangaza kifo cha Padre Maurus Shemdoe kilichotokea Agosti 1, 2023 Hospitali ya Mkoa ya Songea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mhashamu Askofu Mkuu Dallu maziko ya Padre Shemdoe yatafanyika Agosti 5,2023 huko Korogwe Jimbo la Tanga.