Teknolojia mbadala yapunguza gharama ujenzi wa barabara nchini

DODOMA-Matumizi ya Teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja imeweza kupunguza gharama zaidi ya asilimia 50.
Hayo yameelezwa jana na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Maelezo jijini Dodoma.

“TARURA imeweka kipaumbele cha kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi."

Mhandisi Seff amesema hadi kufikia mwezi Machi,2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua.

Ametaja mikoa iliyojengwa madaraja hayo ni Kigoma (92),Singida (24), Tabora (5), Kilimanjaro (10), Mbeya(2),Arusha (6), Morogoro (2), Rukwa(3), Pwani (1), Ruvuma (3) pamoja na Iringa (15).

Aidha, amesema bado wanaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.
“Teknolojia hizo ni pamoja na Ecoroads, Ecozyme na GeoPolymer ambao hadi Sasa kwa kutumia teknolojia ya Ecoroads katika jiji la Dodoma imejengwa Kilomita moja(1) ambayo imekamilika na katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa Kilomita kumi(10),”aliongeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news