NA MATHIAS CANAL
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ushetu wametakiwa kujenga ushirikiano na kuacha vitendo vya majungu na fitina ndani ya chama.

Aidha, wameelezwa kuwa CCM ni chama ambacho kipo madarakani kwa miaka mingi tokea nchi hii ipate uhuru, mikononi mwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hivyo wanapaswa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa kwa mujibu wa katiba husika ili wananchi wasiweze kujengeka na dhana potofu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mheshimimiwa Dkt.Emmanuel Cherehani amesema hayo Agosti 4,2023 wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mapamba.
Amesema kuwa, wanachotakiwa wakae na kujiuliza wametoka na wanakwenda wapi, huku wakiacha tabia za unafiki, uongo na fitina vitendo ambavyo kama wataviendekeza havitawafikisha mbali.


Vilevile Mbunge Cherehani amegawa vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi kwa ajili ya timu za mpira wa miguu katika vijiji vya Kata ya Mapamba kwa ajili ya kuimarisha sekta ya michezo.