Wakumbusheni wananchi kulipa kodi ya pango la ardhi-Dkt.Mabula

KIBAHA-Waziri wa Ardhi Nyumba na Maedeleo ya Makazi,Mhe. Dkt.Angeline Mabula amewasilisha vipaumbele vya wizara yake kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika semina ya uongozi katika Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo kibaha mkoani Pwani. 
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.

Katika wasilisho Agosti 26, 2022, Waziri Dkt.Mabula alizungumzia masuala ya ukusanyaji mapato yatokanayo na sekta ya ardhi, mipango miji pamoja na maeneo ya uwekezaji ambayo yote wakuu hao wa mikoa wanalo jukumu la kusimamia kwenye mikoa yao. 
Dkt.Mabula aliwataka wakuu wa mikoa kusaidia katika kuongeza hamasa katika suala la ukusanyaji mapato ya serikali yatokanayo na sekta ya ardhi. 

"Niwaombe mkasimamie mikakati ya ukusanyaji maduhuli hayo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wananchi waliopo katika maeneo kulipa kodi ya pango la ardhi." 
Sehemu ya washiriki semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani. 

Kwa mujibu wa Dkt.Mabula Rais Samia alitoa msamaha wa riba ya kodi kwa miezi 10 mafanikio yalionekana japo si kwa kiwango kilicho tarajiwa. 

Pia aliwataka wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri katika kutenga fedha katika bajeti za maendeleo ya sekta ya ardhi ili kuhakikisha ardhi inapangwa, kupimwa na kumilikishwa. 
Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifuatilia wasilisho la Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati wa semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

"Halmashauri zitambue kuwa jukumu hilo bado ni la kwao na wanahitaji kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutenga fedha ili kutekeleza majukumu yao na kuwezesha watumishi waliopo katika halmashauri kufanya kazi,"alisema Dkt. Mabula. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news