Wamshukuru Mheshimiwa Simbachawene

DODOMA-Wananchi wa Kata ya Galigali iliyopo Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamemshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kwa ujenzi wa barabara kwa gharama ya kiasi shilingi bilioni 1.4 kwa kumwaga zege katika maeneo korofi. 
Mweyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime akizungumza na Wananchi wa Kata ya Galigali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Pia, wananchi hao wamemshukuru Waziri huyo kwa ujenzi wa madaraja matatu ambayo tangu kukamilika kwake yamewarahisisha mawasiliano kwa kuunganisha kata hiyo na kata zingine 

Shukrani hizo zimetolewa leo na wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti kupitia mikutano ya hadhara ya Waziri huyo anayoendelea kuifanya katika kata hiyo ya Galigali inayoundwa na vijiji viwili ambavyo ni Galigali na Matonya, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika jimbo hilo. 

Imeelezwa kuwa, kata hiyo kabla ya kukamilika kwa Barabara hiyo kulikuwa hakuna Barabara kabisa ya kuunganisha Kata moja hadi nyingine. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wananchi wa Kata ya Galigali, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe. 

Wamesema imekuwa ni msaada mkubwa tangu barabara hiyo ilipokamilika kwani ilikuwa tishio kwa Watumiaji kabla ya kujengwa kwake kutokana na jiografia ya Kata ambayo ipo juu milimani. 

"Kipindi cha masika tulikuwa hatuwezi kusafiri kutoka hapa kwenda Kibakwe Mjini ila kwa sasa tunaweza kusafiri kwani sehemu zote korofi zimeimarishwa kwa kuwekewa zege, Tunamshuru sana Mbunge wetu,"amesema Onesmo Mwanchali Mkazi wa Kata hiyo.

Wamefafanua kuwa licha ya mawasiliano ya barabara kuimarika kwa sasa ila changamoto kubwa inayowakabili wakazi wa Kata hiyo kwa sasa ni kukosekana kwa mawasiliano ya simu na umeme. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akimtambulisha mke wake wakati mkutano wa hadhara katika Kata ya Lumuma ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Wametumia fursa hiyo kumueleza Waziri kuwa mambo mengi yamekuwa yakikwama kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya simu na hivyo wamemuomba ashirikiane na makampuni ya simu kutatua changamoto hiyo. 

Aidha, Wananchi hao wamemuomba Mhe.Simbachawene kupatiwa umeme kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Wamesema Kitendo cha kukosa umeme katika Kata hiyo wamekuwa wakilazimika kutumia vibatari na kulazimika kulala mapema kutokana na giza.
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Galigali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene wakati wa mkutano wa hadhara katika Jimbo la Kibakwe ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

"Mhe.Mbunge tunatambua mchango wako mkubwa wa maendeleo katika Kata hii changa, Tunakuomba utupambanie huko tupate umeme na mawasiliano ya simu ili na sisi tuweze kuboresha maisha kama ilivyo kwa wenzetu,"amesema Diwani wa Kata hiyo Mhe. Mwachayeka Mussa.

Akijibu changamoto hiyo ya umeme na mawasiliano, Waziri Simbachawene amesema suala la umeme atahakikisha ndani ya mwaka huu Kata hiyo inapatiwa na umeme kwani tayari ipo kwenye mpango 

Ameongeza kuwa ujio wa umeme huo utaongeza tija hivyo wananchi wa Kata hiyo wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili pindi umeme huo utakapofika waweze kumudu gharama za kuulipia ili kuingiza majumbani mwao 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mbunge wa Kibakwe ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akikagua Shule ya Sekondari GaliGali ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Kuhusu Mawasiliano ya Simu, Waziri Simbachawene ameahidi kufanya mawasiliano na Makampuni ya simu ikiwemo Mtandao wa Airtel ili waje kuweka mnarav wao kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano.

Aidha, Mhe. Simbachawene ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuubali kutoa fedha kwa ajili ya shule ya Sekondari Galigali pamoja na Barabara hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news