ARUSHA-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia na (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga ametoa rai kwa wananchi,taasisi na wizara kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutembelea vivutio vyetu vya utalii wa ndani.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia na (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akiwa katika picha na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Anderson Mutatembwa alipotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

"Tunamshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa alizozifanya katika sekta ya utalii kupitia filamu ya Royal Tour," alibainisha.
"Tumefika Ngorongoro na tumejionea wageni wamefurika wamekuja kujionea vivutio vya utalii,"alisisitiza.

Aliongeza kwa kusema kuwa, ziara hiyo imeimarisha upendo, uongozi na urafiki kati ya viongozi na watumishi na itaongeza hari ya utendaji kazi.

"Tumekuja kuona Mazingira halisi ya Utalii pamoja na mazingira halisi ya utendaji kazi,tumeona utalii umekuwa kwa kiasi kikubwa wageni ni wengi na sisi kama Serikali tunawajibu wa kuhakikisha tunaweka sera bora za kuwasaidia wageni kuendelea kuja nchini,"alisisitiza.
Aliendelea kusema kuwa, eneo la Ngorongoro ni nzuri, linavutia na Watanzania wana fursa ya kuja kujionea.
Tags
Habari
Maliasili na Utalii
Maliasili za Tanzania
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Ofisi ya Waziri Mkuu