NA MUNIR SHEMWETA
WANMM
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani, Bw. Patrick Kipalu.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.Angeline Mabula (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani, Bw.Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Agosti 2023.
Dkt.Mabula amekutana na mkurugenzi huyo anayeshughulika na Programu za Haki na jitihada za Rasilimali Ardhi katika Bara la Afrika katika ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 29 Agosti 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt.Angeline Mabula (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasilimali kutoka Marekani Patrick Kipalu (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardh,Imaculata Senje jijini Dodoma.
Mazungumzo ya viongozi hao mbali na mambo mengine yamelenga maandalizi ya Kongamano la Nne la Kimataifa litakalofanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 12 hadi 15, 2023 likiwa na ajenda kuu ya upatikanaji wa hatimilki za ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.Angeline Mabula (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani, Patrick Kipalu jijini Dodoma.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
Taasisi hiyo ya Marekani ndiyo wadhamaini wa kongamano hilo linalojadili masuala mbalimbali yahusuyo masuala ya ardhi ikiwemo hati milki za ardhi.