PWANI-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewapa Wakuu wa Mikoa mbinu mbalimbali za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika Mikoa yao.

“Mbinu za kuibua na kutekeleza diplomasia ya uchumi ni nyingi kama vile kufungua balozi, kukusanya taarifa na uchambuzi, majadiliano,.lakini kwenu nyie Wakuu wa Mikoa mnaweza kufanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa mbailmbali za biashara katika mikoa yenu pamoja na elimu kwa Umma,” alisema Dkt. Tax.
“Kupitia mikoa yenu mnaweza mkafanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa za biashara katika mikoa yenu, ninyi ni wadau wakubwa wa kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kuchangia maendeleo,” alisema Dkt. Tax.

“Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya kisheria, kiutendaji na kukuza mazingira wezeshi kushindana kimataifa ambapo ofisi za wakuu wa Mikoa zina nafasi na mchango mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya uchumi, na kuchangia kasi ya maendeleo nchini,” alisema Dkt. Tax.
Waziri Tax aliongeza kuwa Wakuu wa Mikoa ni wadau wakubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kwenye mikoa yao kwani huibua fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika mikoa yao.

Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani yalianza tarehe 21-28 Agosti, 2023.