DODOMA-Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji amefanya mazungumzo na Mhe. Michael Battle, Balozi wa Marekani nchini, leo tarehe 15 Agosti, 2023 jijini Dodoma.
Viongozi hao wamejadiliana kuhusu namna ya kukuza uhusiano na ushirikiano wa uandaaji na utekelezaji wa mipango ya kiuchumi pamoja na kukuza uwekezaji baina ya Marekani na Tanzania.
Aidha, wamekubaliana kuharakisha ukamilishaji wa Jukwaa la Majadiliano (Commercial Dialogue) baina ya Marekani na Tanzania ambalo litakuwa nguzo muhimu ya kuhamasisha Biashara na fursa za uwekezaji.