WRRB yatoa mafunzo utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala

DAR ES SALAAM- Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetoa mafunzo ya utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala nchini.
Mafunzo hayo yanayofanyika kila mwaka nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa kampuni za waendesha ghala,wasimamizi wa Ghala, Meneja Dhamana pamoja na washiriki binafsi.

Aidha, mafunzo hayo yamefunguliwa Agosti 28,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe.Hashim Komba katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mhe. Komba alieleza kuwa, yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa wadau wote nchini.

Vilevile ameitaka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Pia, mafunzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Uendeshaji wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Mary Fidelis.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi za Ghala, Bw.Asangye N. Bangu amesema kuwa,lengo kubwa ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi na matarajio ya mafunzo hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa kwa usahihi kwa kuzingatia sheria .

Aidha,Bangu ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona namna ambavyo watatekeleza shughuli zao za kiserikali.

Pia wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya hivyo, washiriki waliojitokeza kupata mafunzo hayo watapatiwa cheti cha kufudhu usimamizi wa shughuli za uendeshaji ghala ambacho kitatambuliwa na Bodi ya Stakabadhi za Ghala.

"Nilipofanya ukaguzi nilibaini changamoto mbalimbali kwenye maghala, anayeshikiliwa kwanza ni Meneja na Mkurugenzi anakuwa hayupo ukimuuliza Mkurugenzi anakuambia Meneja wangu ndio anayehusika.

"Kwa hiyo, muda mwingine unakuta meneja hana taarifa, hivyo natoa wito kwa washiriki wote kuzingatia mafunzo yanayotolewa ili kuwaongezea uwezo wa kiutendaji,"alisisitiza.

Kwa nini WRRB?

Bodi ya Stakabadhi za Ghala ni taasisi iliyochini ya wizara ya viwanda na biashara. Taasisi hii ilianzishwa chini ya Warehouse Receipts Act No. 10 ya mwaka 2005 na Act No 3 ya 2015 iliyorekebishwa 2016.

Aiha, kazi ya taasisi ni kusimamia na kuhamasisha matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani unaohakikisha usawa na uendelevu wa upatikanaji wa mikopo na mifumo ya masoko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news