MOROGORO-Mtu mmoja amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha magari mawili moja likiwa lori la mizigo na basi la abiria aina ya Tata.

Amefafanua, lori lilikuwa likitokea uelekeo wa Msamvu na kuelekea uelekeo wa Iringa na basi la abiria lililokuwa likitokea Ifakara likielekea katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Msamvu Morogoro na kwamba ajali hiyo imetokea barabara kuu ya Morogoro-Iringa Manispaa ya Morogoro.
Pia Kamanda Ochieng amesema, anayesadikiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa lori na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na wengine sita ambao ni majeruhi walikuwa kwenye basi la abiria na hadi sasa wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.