DAR ES SALAAM-Beki wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Che Malone Fondoh amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia Septemba 24, 2023.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally amesema, beki huyo yupo alipata ajali akitokea Uwanja wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwenda kuwapokea ndugu zake waliokuja kumtembelea wakitokea kwao nchini Cameroon.
“Wakati anarejea nyumbani kwao maeneo ya Mbezi, kufika Mikocheni ndipo alipopata ajali, taarifa zinaeleza alikuwa akimkwepa mwendesha bodaboda na akaingia mtaroni.
“Taarifa njema ni kuwa Che Malone gari aliyopanda ilikuwa na abiria wanne na katika hao hakuna hata mmoja ambaye amepata majeraha makubwa, abiria aliyekuwa amekaa mbele ambaye ni kaka yake yeye ameumia na alikimbizwa hospitali, amepatiwa matibabu na tayari amesharuhusiwa,”amesema Ally.
Amesema beki huyo ambaye ndiye alikuwa dereva wa gari hilo, amefanyiwa vipimo na hajaumia sehemu yoyote.“Yupo salama na kesho atakuwepo mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika.”