RUVUMA-Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro ametoa wito kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kutoa elimu kwa Wachimbaji Wadogo husasan ya vito Wilayani humo ili kuwajengea uwezo kwenye uchimbaji, uchenjuaji na uchukuaji wa sampuli za madini.
Mtatiro ameyasema hayo wakati akipokea Kitabu kinachoonesha Madini yapatikanayo Tanzania kilichoandaliwa na GST kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji kwenye Sekta ya Madini hususan katika tafiti za kina.

Aidha, Mtatiro ameipongeza GST kwa kuandaa na kusambaza Vitabu hivyo ambavyo vitasadia kutambua aina na maeneo gani madini hayo yanapatikana.
Kwa upande wake, Mchumi Mkuu kutoka GST, Osiah Lameck Kajala amepokea ushauri wa Mkuu wa Wilaya na kuahidi kuliweka kwenye mpango kazi wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo unao tolewa na GST kwa maeneo mbalimbali ya nchi
Tags
GST
Habari
Madini Tanzania
Ruvuma Region
Sekta ya Madini Tanzania
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)