MOROGORO-Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) amewasihi Watanzania kuuza ziada ya chalula na kubakisha chakula cha kutosha hadi msimu ujao ili kutokununua chakula hicho kwa bei kubwa zaidi wakati ujao

Waziri Kijaji ameyasema hayo Septemba 15, 2023 akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt.Lugano Wilson.


Vilevile, Waziri Kijaji amebinisha mwenendo wa bei za bidhaa muhimu kwa Septemba 2023 imeonesha bei ya mazao ya mahindi, unga wa mahindi, maharage, unga wa ngano imepungua, viazi mviringo. Sukari himilivu, mafuta ya kupikia na mchele imeongezeka kidogo, wakati bei ya vifaa vya ujenzi kama saruji, nondo na bati imeongezeka kidogo.

Kwa upande wa mikataba ya biashara baina ya Nchi na Nchi (bilateral), Kikanda na Kimataifa, Dkt Kijaji amebainisha kuwa Watanzania wanaweza kuuza bidhaa na huduma katika masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC); Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) pamoja na Nchi kama vile India, Japan, Marekani (AGOA) na China.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amewashauri wakulima na wazalishaji nchini, kuutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ili waweze kupata manufaa na kuongeza tija ya mauzo ya mazao na bidhaa zao kila mkoa nchini.