Dodoma Jiji FC na Mtibwa Sugar walazimishana sare

DODOMA-Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kati ya wenyeji Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar umemalizika kwa sare.

Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao umepigwa Septemba 15, 2023 katika Dimba la Jamhuri jijini Dodoma ambapo Mtibwa Sugar walikuwa wageni.

Abdul Hilary dakika ya 18 aliiwezesha Mtibwa Sugar kuandika bao la kwanza huku Dodoma Jiji likifungwa na Emmanuel Martin dakika ya 38.

Hata hivyo, dakika ya 25 mchezo ulilazimika kusimama baada ya golikipa wa Mtibwa Sugar Mohammed Makaka kudondoka ghafla na kuwahishwa hospitali.

Akizungumza na runiga ya Azam baada ya mchezo kumalizika daktari wa Mtibwa Sugar,Laurence Mushi amesema, hali ya Makaka inaendelea vizuri kwa sasa kinachosubiriwa ni majibu ya vipimo kujua tatizo ni nini.

Dkt.Mushi amesema, mlinda mlango huyo alianguka ghafla pasipokua na mpira wowote wa kugombania. "Baada ya kumuangalia nikagundua amepoteza fahamu, tukamuwahisha hospitali, kwa sasa anaendelea vizuri, lakini tunasubiri majibu ya vipimo vya hospitali."

Aidha, kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inafikisha alama nne huku Mtibwa Sugar wanatimiza alama mbili tu baada ya wote kucheza mechi tatu katika ligi hiyo yenye mvuto wa aina yake nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news