Jeshi la Polisi kufanya tathimini

DAR ES SALAAM-Jeshi la Polisi nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Maafisa wakuu waandamizi kutoka Makao Makuu, Mikoa na vikosi kuanzia Septemba 04, 2023 jijini Dae es Salaam kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akitoa taarifa hiyo Septemba 02,20223 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema,mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Misime amebainisha kuwa, katika mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalam kutoka vyuo vya hapa nchini na wataalam wa kada mbalimbali.

Amesema, maafisa washiriki watapata fursa ya kufanya tathmini ya majukum ya Jeshi la Polisi na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa mwaka 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, SACP Misime amesema kuwa, mikutano hiyo ni utaratibu uliowekwa na Jeshi la Polisi ili kuwakutanisha maafisa wakuu waandamizi pamoja kufanya tathmini na kuweka mikakati ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa nchini.

Misime ameongeza kuwa, mkutano huo utaongozwa na kauli mbiu isemayo, Matumizi ya TEHAMA kuleta uwazi na ufanisi katika utendaji wa Jeshi la Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news