IRINGA-Leo Septemba 10, 2023 Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu wa Jimbo Katoliki Iringa ameadhimisha Jubilei ya miaka 50 tangu alipowekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Upadre sanjari na Jubilei ya Miaka 125 tangu Wamisionari wa kwanza walipofika jimboni humo mnamo mwaka 1896.

Misa Takatifu imefanyika katika viwanja vya Kichangani vilivyopo pembezoni kidogo na Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu - Kihesa Jimbo Katoliki Iringa.