Kibangu watoa msaada kwa wagonjwa Muhimbili

DAR ES SALAAM-Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kutoka kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kibangu iliyoko Manispaa ya Ubungo.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Redemptha Matindi ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Ukunga na Uuguzi amewashukuru kwa kuguswa na kujali kwani mahitaji ni mkubwa na si jambo jepesi kuwafikia wote.

“Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuhudumia wananchi wake lakini wahitaji ni wengi kwa hiyo sisi kama jamii tunao wajibu wa kuisaidia, pia tunawaomba wanajamii wengine wajitokeze na kusaidia wezetu,” amesema Bi. Redemptha.

Kwa upande Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kibangu, Bw. Desdery Ishengoma amesema vitu hivi vimekusanywa kutoka kwa wananchi mbalimbali wanaoishi Kibangu na maeneo jirani ambao waliguswa na kuweza kutoa msaada huo.

“Tumeguswa na tumeona ni vyema kutoa msaada huu Muhimbili kwa wagonjwa ambao hawana ndugu hospitalini hapa ili wajisikie kama wenzao, kwani wagonjwa wa leo ndio wazima wa kesho na wazima wa leo ndio wagonjwa wa kesho,”amesema Bw.Ishengoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news