DAR ES SALAAM-Hospitali ya Taifa Muhimbili imejumuisha lugha ya alama ili kutoa usaidizi kwa wagonjwa wenye tatizo la kusikia ili kuwaondolea changamoto za mawasiliano wakati wa kupata huduma za matibabu hospitalini hapa.

“Kama mnavyotambua lugha ya alama ndio njia pekee ya mawasiliano kwa watu wenye changamoto za kusikia ndio maana uongozi umeona ipo haja ya kuwa na wataalam wa lugha ya alama ambao watakuwepo maeneo yote ya kutolea huduma na kuendelea kusambaza ujuzi kwa wataalam wote ili kurahisisha mawasiliano,”ameongeza Dkt.Nkya.
Dkt. Nkya amebainisha kuwa huduma hii inapatikana siku zote za kazi kwa wananchi wote waliopo ndani na nje ya Muhimbili ambao wanachangamoto hiyo.