DAR ES SALAAM-Madaktari wazawa Hospitali ya Taifa Muhimbili wanaendelea kufanya upasuaji wa kupandikiza figo ambapo wagonjwa 12 kuanzia Septemba 27,2023 watapata huduma hiyo sita kati yao watafanyiwa Upanga kwa njia ya kawaida na sita watafanyiwa wiki ijayo huko Mloganzila kupitia mfumo wa matundu madogo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali hiyo, Dkt. John Rwegasha amesema huu ni mwendelezo wa utoaji huduma za kibingwa nchini unaofanywa na madaktari wazawa ambao sasa wana ujuzi wa kutoa huduma hizo.
