
Mke wa Rais wa Zanzibar,Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutoa mada juu ya nafasi ya mwanamke katika kilimo wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula barani Afrika kwa mwaka 2023(AGRF) Septemba 6,2023 linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu).
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Mkutano wa Kimataifa unaojadili Mfumo wa Chakula,unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kulia kwake ni Waziri wa Maendeleo anayeshuhulikia Masuala ya Kimataifa wa Norway, Mhe.Anne Beathe Tvinnereim na kushoto kwake ni Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani barani Afrika ( AGRA) Dkt.Agnes Kalibata.
Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa Unaojadili Mfumo wa Chakula, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

