Mpunga na mahidi yetu tunatamani wanunue kwa dola-Malekano

NA GODFREY NNKO

AFISA Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX),Godfrey Malekano amesema, litakuwa jambo la faraja iwapo wafanyabiashara kutoka nchi jirani watanunua mahindi na mpunga hapa nchini kwa kutumia dola.
"Lakini kama Mheshimiwa Waziri wetu alivyosema kuna miradi mingi ya kimkakati ambayo inaendelea kutekelezwa hapa nchini ikiwemo Bwawa la Mwalimu Nyerere na Reli ya Kisasa, hivyo tunahitaji dola, kwa hiyo tunapopata dola nyingi zaidi tunaweza ku-cover masuala kama hayo."
 
Malekano amesema, hatua hiyo si tu itasaidia Taifa kukabiliana na upungufu wa fedha za kigeni ambao unazikumba nchi mbalimbali duniani kwa sasa, bali utazidi kuimarisha akiba ya fedha za kigeni nchini na kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati.

Ameyabainisha hayo leo Septemba 7, 2023 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

TMX ni taasisi ya 11 tangu vikao kazi hivyo vianze ambapo, mashirika, taasisi za umma zinapata nafasi ya kueleezea zilipotoka, zilipo na zinakoelekea kwa ustawi bora wa umma na Taifa.

"Lakini pia haya mahindi au mpunga tungependa na sisi tupate dola kama wanavyofanya kwenye mifugo, watu wanatoka Kenya kuja kununua mifugo hapa Tanzania kwa kutumia shilingi wanavuka mipaka wanaingia, lakini wenyewe wanapeleka Uarabuni, wanakwenda kuuza kwa dola.

"Kwa sababu sisi tunaponunua mbolea au viuatikifu tunalipa kwa dola nje, ni vizuri hata wanaokuja kununua wakalipa kwa dola na ili lifanyike ni lazima mazao yakae kwenye maghala."

Amesema, ili haya yaweze kufanikiwa kwa ufanisi ni wakati wa Serikali na wadau mbalimbali kuwekeza katika maghala ya kisasa ambayo yatawezesha mifumo kama yao ifanye kazi, pia kuwe na ubora wa bidhaa unaotakiwa na kuthibitika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news