NA FRESHA KINASA
JIMBO la Musoma Vijijini mkoani Mara chini ya Mbunge wake, Prof. Sospeter Muhongo limeendelea kurekodi mafanikio ya aina yake katika sekta mbalimbali.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge leo Septemba 19,2023.1a. Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.
"Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne,"amefafanua Prof.Muhongo.
1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo , ANROADS mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango.2a. BONDE LA BUGWEMA
Kupitia taarifa hiyo, katika kuelekea kilimo cha umwagiliaji, mshauri ameanza kufanya upembuzi yakinifu kuanzia Septemba 17, 2023 hadi Oktoba 16, 2023.
"Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema. Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga,"amebainisha Prof.Muhongo.
2b. BONDE LA SUGUTI
Pia, katika bonde hilom,mshauri ataanza kufanya upembuzi yakinifu baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema
3a. ELIMU YA SEKONDARI-MAABARA
"Tunaendelea na ujenzi wa maabara tatu (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa.
"Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara tatu kwenye kila sekondari yetu ya kata kwa sasa tunazo 25 na tunajenga mpya tano. Sekondari za binafsi nimbili,"amefafanua Prof.Muhongo.
3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
"Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.
"Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa science high school ni maji ya bomba, maabara tatu, bweni, na bwalo la chakula.
"Lengo letu ni mwakani, 2024 jimbo letu liwe na angalau high schools mbili hadi tatu za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya sanaa."
3c. ELIMU YA MSINGI-MRADI WA BOOST
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shule za msingi tisa zimepewa jumla shilingi bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.
"Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana."
Aidha,shule za msingi zilizopewa fedha ni Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B.
MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu. "MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha."
"Vilevile, MUWASA imewasilisha serikalini bajeti ya kutekeleza mradi huu.MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi.
"Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama."
4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
Pia,ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa.
4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maji ya bomba kwenye kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama.
Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka."Tenki la ujazo wa lita 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani."
4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama.Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.
"Tenki la ujazo wa lita 500,000 limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo kutoka ofisi ya Mbunge la Jimbo la Musoma Vijijini.
4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa, maji ya bomba ya kata hizi mbili yatatoka kwenye tenki ya lita 500,000 liliojengwa Mlimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama.
"RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya kata hizi itaanza kujengwa."
4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji.Ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi.
4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
"Ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru.Mabomba yanaelendelea kutandazwa.Maji kutoka kwenye tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (kata jirani ya Bugwema),"
4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
"Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya wazaliwa wa Rusoli kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki. RUWASA imekamilisha ujenzi wa tenki la lita 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo."
5.AFYA
"Hospitali ya halmashauri yetu yenye hadhi ya hospitali ya wilaya imeanza kutoa huduma za afya hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.
"Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen."
5b. VITUO VYA AFYA
Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa).
5c. ZAHANATI
"Tuna jumla ya zahanati 42. Zahanati 24 zinatoa huduma za afya vijijini mwetu,zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
"Zahanati nne za binafsi zinatoa huduma za afya vijijini mwetu.Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji umeme vijijini mwetu (REA na TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni.
"Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA na TANROADS).Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA na MUWASA)."
SHUKRANI
"Ninatoa shukurani nyingi kwa Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na wadau wengine wa uchangiaji wa maendeleo na ustawi wa jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana,tafadhali endeleeni kutuunga mkono."