SINGIDA-Mwandishi wa habari,Mathias Canal amechangia madawati 30 yenye thamani ya shilingi milioni 2.1 na vitakasa mikono 20 vyenye thamani ya shilingi milioni 1.4.

Pamoja na mambo mengine pia Mathias amechangia kwa kutoa motisha ya shilingi 500,000 kwa ajili ya walimu katika shule hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kuwafundisha wananfunzi shuleni hapo.
Kadhalika amesema kuwa, atawasomesha watoto wote watakaomaliza darasa la saba na kupata ufaulu wa alama ‘’A’’ kwa kila somo kuanzia wale waliohitimu mwaka huu 2023 katika shule hiyo.

Ameongeza kuwa, wanafunzi hao bado hawajamaliza elimu ya darasa la saba mpaka pale watakapopata matokeo ya mitihani waliyoifanya, hivyo wazazi na walenzi wanapaswa kuendelea kuimarisha ulinzi na mwenendo bora wa malezi kwa watoto hao.
Wakati huo huo,Mathias Canal ameipongeza Serikali kwa kutoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu.
Katika mahafali hayo, Mathias Canal aliambatana na Diwani wa Kata ya Kiomboi, Mhe. Omary Omary, na Mkurugenzi wa DM PLANET,David Mtengile ambaye amechangia 100,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu.