Mwimbaji wa nyimbo za injili mbaroni, mwalimu afariki Mbeya

MBEYA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwimbaji wa nyimbo za injili, SIFA BONIVENTURE BUJUNE (25) Mkazi wa Isyesye JJjini Mbeya kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi na kuurusha kwenye mitandao ya kijamii.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga.

Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 13, 2023 huko Isyesye Jijini Mbeya baada ya kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuusambaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kurusha maudhui wa Youtube. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Wakati huo huo, Kamanda huyo amesema, Septemba 14, mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi huko katika nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari Mtanila iliyopo Kijiji cha Igangwe Wilaya ya Chunya, Mkuu wa Shule hiyo aliyefahamika kwa jina la MAGWIRA NKUTA (41) alifariki dunia baada ya kunywa kimiminika kinachodhaniwa ni sumu.

"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo kwani inadaiwa kuwa kabla ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru, marehemu alikabidhiwa fedha na ofisi ya TAKUKURU kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kibao cha “KLABU YA TAKUKURU RAFIKI SHULENI” lakini pamoja na kutumiwa fedha hizo hakuweza kutengeneza kibao hicho hadi Mwenge wa Uhuru ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wa Klabu hiyo.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi walioibiwa mali mbalimbali kufika kituo cha Polisi Rujewa, Mbeya Mjini na Chunya kwa ajili ya utambuzi wa mali zao. Aidha, linatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wakamatwe na kuchukulia hatua za kisheria."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news