Nendeni mkatangaze fursa zilizopo nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka mabalozi walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kuitangaza Zanzibar.

Ni katika fursa za sekta ya utalii, uwekezaji, ufadhili wa masomo, misaada ya teknolojia, mikopo yenye masharti nafuu, kuitangaza sera ya uchumi wa buluu na fursa za kibiashara na soko la bidhaa za ndani za viungo likiwemo zao mama la karafuu.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Septemba 5,2023 alipokutana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali akiwemo Mhe.Joseph E.Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Canada.

Mhe.Fatma M.Rajab, Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe.Naimi S.H.Aziz ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe.Ali Mwadini, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mhe.Ceasar Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia ambao walifika Ikulu jijini Zanzibar kujitambulisha na kumuaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news