Ole wao wanaoshambulia askari, watakiona-Polisi

DAR ES SALAAM-Jeshi la Polisi Tanzania limetoa onyo kali kwa watu ambao wamekuwa na tabia za kuwashambulia askari wakati wakitekeleza majukumu yao.

Onyo hilo limetolewa leo Septemba 13, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David A.Misime.

"Askari polisi wanapotekeleza majukumu yao wameruhusiwa na sheria kubeba silaha ili waweze kulinda maisha ya watu na mali zao, kulinda maisha yao na mali za Serikali ikiwepo hiyo silha aliyobeba.

"Kumejitokeza mtindo wa baadhi ya watu ambao wamevunja sheria na wakati mwingine wanatenda uhalifu wa kujichukulia sheria mikononi, wanawashambulia askari wakiwa wamebeba silaha.

"Jeshi la Polisi linawataka watu wa aina hiyo kuacha tabia hiyo, kwani askari ni binadamu kama binadamu mwingine na sheria inamruhusu kutumia silaha hiyo kulinda uhai wake, uhai wa mtu mwingine na mali za huyo mtu na mali za Serikali.

"Hivyo, wenye tabia hiyo waache mara moja na wale ambao wamewahi kufanya hivyo wafahamu lazima watakamatwa na kufikishwa mahakamani, kwani wametenda uhalifu."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya SACP Misime, Jeshi la Polisi Tanzania kwa mujibu wa sheria za nchi limepewa jukumu la kulinda maisha ya watu na mali zao.

Aidha, utekelezaji wa jukumu hilo linapata mafanikio makubwa siku hadi siku kutokana na ushirikiano wa vyombo vingine vya dola, wadau wengine wa ndani na nje kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wananchi wapenda amani, mshikamano na watii wa sheria za nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news