Rais Dkt.Mwinyi aelekea Cuba kushiriki G77+China

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea Havana nchini Cuba kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la 77 na China (G77+ China) utakaofanyika tarehe 15 hadi 16 Septemba 2023.

Mkutano huo unalenga kukutanisha Mataifa yanayoendelea (Developing Countries) ili kujadili changamoto zinazoikabili dunia hasa baada ya kuathirika na UVIKO-19 na migogoro inayoendelea duniani pamoja na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi.

Hivyo, mkutano huo utajikita zaidi katika kutafuta namna bora ya kujenga ustahimilivu kupitia maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu ili kundi la G77 na China liweze kufikia malengo yake kwa pamoja.

Mkutano huu utaongozwa na kaulimbiu isemayo “Current Development Challenges: The Role of Science, Technology and Innovation”.

Rais Dkt.Mwinyi anatarajiwa kuhutubia mkutano huo na kuelezea vipaumbele vya Tanzania, pamoja na hatua zilizochukuliwa kukuza tafiti na kuimarisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu (STI) katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news