Rais Dkt.Samia ateua, aridhia uteuzi TFRA, CPB, AGITF, COPRA, NARCO na NFRA

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameteua na kuridhia uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 29, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ambapo Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameteua wafuatao;

i) Amemteua Bw. Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority-TFRA).Kabla ya uteuzi Bw. Laurent alikuwa Mhadhiri, Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania).

ii) Ameridhia uteuzi wa Bw. Patrick Magologozi Mongella kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Board-CPB). Bw. Mongella ni Mkurugenzi wa Miradi, Benki ya Maendeleo TIB.

iii) Ameridhia uteuzi wa Bi. Mwanahiba Mohamed Mzee kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Inputs Trust Fund-AGITF). Bi. Mwanahiba aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania.

iv) Ameridhia uteuzi wa Bi. Irene Madeje Mlola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Regulatory Authority-COPRA). Bi Mlola aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Financial Sector Deepening Trust (FSDT).

v) Ameridhia uteuzi wa Dkt. Andrew Marcelin Komba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Authority-NFRA). Bw.Komba ni Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais.

vi) Ameridhia uteuzi wa Bw. Felix H. Mlaki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company Limited-NARCO). Bw. Mlaki ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya NARCO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news