Rais Dkt.Samia atoa miezi sita TANESCO

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amempa miezi sita Mkurugenzi mpya wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Gissima Nyamo Hanga.
Viongozi mbalimbali wakila Kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

Ni kwa kumtaka ahahakikishe anasimamia ukarabati wa mitambo ya umeme inayosababisha changamoto ya uwepo wa mgao wa umeme nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

“Nenda kaanzie pale Maharage alipofikia, najua utaweza, nakupa miezi sita nakuangalia pale TANESCO, kazi yako ya kwanza ni kusimamia ukarabati wa hiyo mitambo.

“Tuna changamoto kama taifa si ya mtu, mtu mwingine anaweza kusema Maharage kwa sababu ya kukatika katika kwa umeme kaondoshwa, hapana si sababu yake;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

Amesema kuwa, baada ya kipindi hicho hatakuwa tayari kusikia suala la mgao kwa kuwa suala la umeme linagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameyasema hayo leo Septemba 26, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uapisho wa viongozi aliowateua hivi karibuni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Mohamed Jumanne Gombati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

Ameeleza sababu inayosababisha uwepo kwa mgawo wa umeme ni kuwepo kwa mitambo ambayo kwa muda mrefu haijafanyiwa matengenezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Said Othman Yakubu kuwa Balozi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

“Ikiwa haitafanyiwa huduma mitambo hii kwa pamoja ni lazima mitambo mingine iwake mingine izime. Kwa hiyo tuna upungufu wa umeme,”amesema Mheshimiwa Rais.

Kuhusu uhamisho wa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Maharage Chande ambaye alihamishwa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kupelekea Shirika la Mawasiliano (TTCL) na jana kuteuliwa kuwa Postamasta Mkuu, amesema hali hiyo ni kawaida katika utendaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. John Ulanga kuwa Balozi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

Rais Dkt.Samia amesema, sababu ya kumtoa kiongozi huyo kutoka Shirika la Mawasiliano (TTCL) kwenda kuwa Postamasta Mkuu, kuwa ni baada ya kubaini kuwa kiongozi huyo ana biashara ndani ya shirika hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

“Niliona sekta ya TTCL ingekufaa zaidi, baadaye nikagundua una biashara ndani ya TTCL na kwa sababu kampuni ile inafanya vizuri nikasema hapana, usiende pahala ambapo unafanya biashara nikaona sasa nikupe uposta Masta Mkuu."
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news