IRINGA-Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego amesema, mfumo unaotumiwa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wa kugawa Vitabu vya Madini yapatikanayo Tanzania kwa wakuu wa mikoa na wilaya,

Dendego amesema hayo leo Septemba 17, 2023 Ofisini kwake mkoani Iringa baada ya kupokea Vitabu hivyo ambavyo ni nakala ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya za Iringa, Kilolo na Mufindi kutoka kwa Meneja wa Sehemu ya Jiolojia wa GST Maswi Solomon.
Aidha, Dendego ameipongeza GST kwa kuandaa kitabu hicho ambacho kikitumiwa vizuri kitakuwa mwarobaini kwa Wachimbaji Madini hususan kwa wale wanaochimba kwa kubahatisha sambamba na kuvutia uwekezaji hasa utafiti wa kina kwenye maeneo yaliyoainishwa na GST.
Pamoja na Mambo mengine, Dendego ametoa wito kwa GST kwa kuzingatia umuhimu wa kazi zake ni vyema kushiriki "Kongamano la Utalii Karibu Kusini" litakaloenda sambamba na maonesho mbalimbali ikiwemo Madini linalolenga kuifungua Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini hususan katika maana nzima ya Utalii.
"Naomba nichukue fursa hii kuwapongeza GST kwasababu mmekuja katika kipindi mwafaka, Mkoa wa Iringa umeandaa Kongamano la siku tano litakalo lenga kuifungua Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini, hivyo nawaomba sana GST mshiriki ili muweze kutusaidia kujibu maswali mbalimbali yatakayo ulizwa na Wawekezaji tuliowaalika," amesema Dendego.
Kwa upande wake, Meneja kutoka GST Maswi amesema ugawaji wa Vitabu hivyo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa Jijini Mwanza katika Kongamano la Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA) lililofanyika Jijini Mwanza.
Sambamba na hayo, Maswi amefafanua kuwa Mkoa wa Iringa unayo madini mkatati akitolea mfano Mbale za Bauxite zinazozalisha Alumina na Aluminium muhimu kwenye viwanda vya bidhaa za kimkakati ikiwemo vya teknolojia.

Ni kutokatana na mabadaliko ya jiolojia kwenye maeneo ya mkoa huo akitolea mfano Isimila Natural Stone Pillars ambazo pia zilitajwa kwenye kitabu hicho.
Tags
Habari
Madini Tanzania
Sekta ya Madini
Sekta ya Madini Tanzania
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)