Ripoti itakapokamilika itasaidia kuandaa sheria, sera ya jinsia-Siti

NA SALMA LUSANGI
WMJJWW

MkURUGENZI wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Siti Abbas Ali amesema, ripoti ya tafiti ya Jinsia, Maambukizi ya virusi vya UKIMWI na Haki za Binadamu inayotekelezwa na idara hiyo itakapokamilika itasadia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupanga Mipango, Sera na Sheria ambazo zitazingatia masuala ya kijinsia.

Akizungumza wakati akifunga kikao cha uwasilishaji wa ripoti ya awali ya tafiti hiyo katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa ZURA, Maisara, Unguja amesema, ripoti hiyo itakapokamilika itasaidia Serikali kuandaa sheria, sera ya jinsia pamoja na kusimamia haki za wanawake waliopata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Amesema, mara nyingi wanawake wakipatwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI huwa hawataki hata kuajiriwa wakati Katiba ya Zanzibar (1984) imetoa uhuru kwa kila mtu kushiriki katika mambo ya msingi ikiwemo haki ya kuajiriwa, kupata matibabu, elimu na kadhalika.

Pia amesema Sheria ya Ajira namba 11 ya mwaka 2005 imetoa ufafanuzi masuali ya ajira kwa mtu aliyepata maambukizo ya virusi vya UKIMWI.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Siti Abbas Ali akifunga kikao cha Uwasilishaji ripoti ya awali ya Utafiti wa Jinsia, Maambukizi ya virusi vya ukimwi na Haki za Binadamu kilichofanyika mwisho wa wiki, katika ukumbi wa ZURA Maisara Unguja.

“Ripoti hii itakapo kamilika itasaidia kuongeza nguvu ya kuziangalia sheria zetu kama zinamapungufu kuongeza nguvu ya kuzifanyia marekebisho kwa mara nyingi wanawake wanapopata maambukizi wanakuwa wanaona tabu kufuatilia haki zao.

"Kwa mfano haki ya kupata ajira, haki ya kupata elimu. Anapotaka kuendelea na elimu ya juu anahisi ameshaambukizwa kuna haja gani ya kuendelea na amsomo? Lakini utafiti utakapomalizika basi itamsaidia yule mwanamke kuweza kuzitambua haki zake,”alisema Siti.

Aidha, alisema Idara yake kila wiki inafanya zoezi la kutoa elimu katika makundi mbali mbali ikiwemo madrasa za dini, skuli, makundi ya watu wenye ulemavu n.k kuhusiana na udhalilishaji, athari za mimba za utotoni, maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kadhalika, ili jamii wafahamu kwamba athari zake zinaathiri kimwili na kisaikolojia.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abbas Ali (kati) akiwa katika picha ya pamoja baada kufunga kikao cha Uwasilishaji ripoti ya awali ya Utafiti wa Jinsia, Maambukizi ya virusi vya ukimwi na Haki za Binadamu kilichofanyika mwisho wa wiki, katika ukumbi wa ZURA Maisara Unguja.

Kwa upande wake mtafiti ambaye ndiye muwasilishaji wa ripoti ya awali, Bi.Lorraine Kiswaga amesema, katika utafiti huo umewafikia makundi 15 kwa Unguja na Pemba kupitia wilaya zote 11 ikiwemo kundi la watu walioathirika, watumiaji dawa za kulevya, watu wenye ulemavu n.k.

Amesema, utafiti huo umeanza mwezi Mei, 2023 na upo katika hatua za mwisho ambapo pia wameangalia jinsi gani wanawake walioathirika wanaweza kutumia huduma ya afya iliyopo hasa huduma ya afya ya uzazi. Pamoja na kuangalia kundi gani limeathirika zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news