Serikali yataja faida za Samia Bus Terminal Mkuranga

MKURANGA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa amemueleza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo kuharakisha upatikanaji wa fedha kiasi cha Sh. bilioni 38 kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya Mkuranga itakayofungua fursa kwa wananchi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo Septemba 12, 2023 alipokuwa akikagua eneo la Kipala Mpakani, Kata ya Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani litakalotumika kujenga stendi hiyo itakayoitwa ‘Samia Bus Terminal Mkuranga’.

“Nimekuja kukagua na kujionea eneo la ujenzi wa stendi hapa Mkuranga, niwapongeze kwa hatua ambazo mmeanza kuchukua kwa kutenga eneo ambalo Stendi itajengwa, namuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuhakikisha fedha hizi zinapatikana na zinaletwa hapa Mkuranga ili kujenga stendi hii itakayofungua fursa za uchumi, kuleta ajira na kutoa huduma bora ya usafiri wa Mikoa ya Kusini,”amesema.

Akizungumzia jina ambalo wananchi wa Mkuranga wameliainisha kwa ajili ya Stendi hiyo kuwa ni SAMIA BUS TERMINAL amesema maoni hayo yatawasilishwa kwa Mamlaka ili akiridhia stendi itakapokamilika iweze kuitwa jina hilo lililopendekezwa na wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nasri Ali akimpitisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa katika mchoro unaoonesha ramani ya kituo cha mabasi kitakachojengwa Mkuranga katika eneo la Kipala Mpakani-Mwandege.

Naye, Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega amesema eneo hilo lina ukubwa wa ekari 49 na halina mgogoro wowote na wananchi wamelilinda kwa muda mrefu kwa ajili ya kujengwa stendi hiyo.

‘Sisi tuko tayari kutafuta wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa majengo makubwa karibu na stendi hiyo, nyumba za kulala wageni na biashara zingine ili Stendi hiyo ikikamika hapa Mkuranga pachangamke kibiashara’ alisisitiza Mhe. Ulega.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Hassanal amesema kwa kipindi kirefu wananchi wa Mkuranga wametaabika kwa kukosa stendi ya uhakika na kwamba eneo hilo litakapojengwa stendi itakuwa ya kisasa yenye maegesho ya mabasi, malori, maeneo kupumzikia abiria pamoja na eneo ya wajasiriamali wadogo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news