DODOMA-Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limetakiwa kukamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa miundombinu ya umeme wa chini unaoendelea katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi akizungumza na Mhandisi wa TANESCO, Richard Kafura wakati akikagua mfumo wa ujenzi wa miundo mbinu ya umeme katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa Septemba 21, 2023 na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt.Jim Yonazi alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba.
Dkt.Yonazi alisema kuwa,TANESCO wana jukumu la usimamizi wa karibu na ulazima katika ujenzi wa miundombinu ya nishati ya umeme katika Mji wa Serikali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi akizungumza na Mhandisi wa TANESCO, Richard Kafura wakati akikagua mfumo wa ujenzi wa miundo mbinu ya umeme katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Amesema,baada ya muda mfupi ujao mahitaji ya umeme yatakuwa makubwa kutokana na Agizo la Serikali kuzitaka ofisi zote za Serikali jijini Dodoma kuhamia Mtumba mapema ifikapo Januari Mosi, mwakani.
Sambamba na hilo Dkt.Yonazi amelitaka shirika hilo kuvipa vipaumbele viwanda vya ndani kwa kununua bidhaa zinazofaa kununuliwa nchini katika viwanda hivyo.
“Mnafahamu kuwa kuna changamoto ya kiuchumi duniani kote, hivyo hatuwezi kununua nje kila kitu, vitu ambavyo vinaweza kununuliwa ndani ya nchi vununuliwe ndani ya nchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu, Dkt,Jim Yonazi akizungumza na Msimamizi Mkuu wa miradi ya Ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Mhandisi Anania Saudeni, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
"Ili kupunguza upelekaji wa fedha za Tanzania nje, ni vizuri kuhusisha viwanda vya ndani ambavyo vinawezekana kutoa huduma vitoe huduma,”alifafanua Dkt.Yonazi.
Akiendelea kusisitiza kuhusu suala la ubora na muonekano wa ujenzi unaoendelea katika Mji wa Serikali, Dkt.Yonazi alisema, ni muhimu kuzingatia maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya huduma nyingine.
Dkt.Yonazi alitolea mfano miundombinu ya umeme,maji na mawasiliano na kutoa wito kwa kila Mkandarasi katika eneo kufuata mpango kazi ambao ulikuwa umewekwa, na alisisitiza suala zima la kuzingatia muda wa umaliziaji wa kazi.
“Tunakumbuka agizo la Serikali linataka watumishi kuhamia Mtumba ifikapo tarehe 1 Januari 2024, hivyo ni muhimu kuhakikisha kwamba majengo yanakwenda vizuri katika umaliziaji na kuweka huduma ambazo ni muhimu,” alibainisha.
Akiongea katika ziara hiyo, Mhandisi Richard Kafura kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) alisema,ujenzi wa mradi huo unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi DERMO Contruction Limited.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu, Dkt,Jim Yonazi akizungumza na Msimamizi Mkuu wa miradi ya Ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Mhandisi Anania Saudeni, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Ambapo mpaka sasa ujenzi wa mifereji ya kupitishia miundombinu ya umeme na mfumo wa umeme wa ardhini unaendelea kutekelezwa na mkandarasi.