ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na upandaji wa bei za vyakula hasa mchele na sukari nchini.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Septemba 25, 2023 Ikulu jijini Zanzibar wakati akizungumza na wafanyabiashara wanaoagiza vyakula nje ya nchi na watendaji wa Serikali.
Amesema, matarajio ya Serikali ni kurudisha bei za awali kwa bidhaa zilizopo madukani, pia ameagiza Serikali kutoa fedha zake za kigeni na kuwapa kipaumbele wafanyabiashara hususani waagizaji vyakula nje ya nchi, hivyo amewataka wafanyabiashara hao kushirikiana kuagiza bidhaa hizo kwa pamoja.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amegusia suala la mizigo kushukia Bandari ya Mkoani ili kupunguza gharama za bidhaa Pemba.