Tanzania, Ireland zakubaliana Sekta ya Michezo

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.Damas Ndumbaro amekutana na Balozi wa Ireland hapa nchini Mhe. Mary O' Neill na kukukubaliana kushirikiana katika Sekta ya Michezo hususani soka la wanawake pamoja na Sekta ya Sanaa katika eneo la uchoraji.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Septemba 22, 2023 ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam,Waziri Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewasilisha ombi kwa nchi hiyo isaidie kutoa mafunzo kwa watalaamu wa michezo hapa nchini katika eneo la usimamizi wa miundombinu ya michezo pamoja na wataalamu wa kufundisha michezo.

"Nawakaribisha katika nchi yetu muweze kufanya maandalizi ya misimu ya ligi zenu kwa kuwa nchi yetu ina maeneo mazuri hapa Dar es Salaam-Kigamboni, Tanga, Arusha na Zanzibar.

"Ninaamini mtafurahia sana na sasa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17 ya nchini Morocco ipo hapa Tanzania ikiwa inacheza mechi za kirafiki na timu yetu ya umri huo,"amesisitiza Mhe. Ndumbaro.

Kwa upande wake Balozi huyo Mhe. MaryO' Neill amekubali maombi hayo na kuahidi kuwa mwezi Novemba , mwaka huu atakuja msanii nguli wa fani ya uchoraji, Mick O'Dea ambaye atatoa uzoefu kwa wasanii wa hapa nchini akibainisha kuwa wizara imemkaribisha ashirikiane na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo katika fani hiyo kwa kuwa ni taasisi bora inayotoa mafunzo kwenye eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news