BONN-Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesisitiza kuendelea kusimamia matumizi salama ya kemikali na taka zitokanazo na kemikali ili kuzuia athari kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa Septemba 29, 2023 jijini Bonn nchini Ujerumani na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt.Grace Magembe wakati akiwasilisha tamko la Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Usimamizi wa Matumizi Salama ya Kemikali Duniani (ICCM5) kwa niaba ya Mhe.Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Dkt.Magembe alieleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuchukua hatua madhubuti kudhibiti matumizi mabaya ya kemikali.
Lengo ni kuhakikisha usalama wa wananchi na mazingira nchini kwa kutekeleza kwa vitendo malengo endelevu ya maendeleo ya Dunia na katika kujenga uchumi endelevu wa nchi.
“Pamoja na kuwa matumizi ya kemikali ni muhimu na zipo faida nyingi zitokanazo na kemikali hasa katika sekta za Afya, Kilimo, Elimu, Viwanda na nyinginezo.
"Shughuli za kemikali zisiposimamiwa vizuri, zinaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya binadamu,mazingira, usalama mahala pa kazi, ulinzi na usalama wa nchi,”amesema Dkt.Magembe.
Pia, Dkt.Magembe amesema kuwa, takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha, takribani vifo milioni mbili duniani kwa mwaka vinatokana na matumizi mabaya ya kemikali yakiwemo madhara mengine kama ulemavu, kuharibika kwa mimba, magonjwa ya mfumo wa hewa na saratani.
Sambamba na hilo Dkt.Magembe amebainisha mipango ya Tanzania katika matumizi ya kemikali hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uratibu na usimamizi wa kemikali ndani ya nchi.
Pamoja na kutenga rasilimali za kutosha ikiwemo fedha ili kuwezesha utekelezaji wa mpango mkakati huo hususani kuziwezesha nchi zinazoendelea kuzuia na kudhibiti madhara yatokanyo na matumizi ya kemikali.
Dkt.Magembe ameziomba nchi zilizoendelea kushirikiana na nchi zinazoendelea katika kuwekeza kwenye teknolojia za kisasa kwenye viwanda vinavyozalisha dawa, vifaa tiba, mbolea, viuatilifu na bidhaa nyinginezo kwa lengo la kuzalisha bidhaa rafiki kwa afya ya binadamu na mazingira na pia kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa hizo.