NA KASSIM NYAKI
NCAAJAMHURI ya Muungano wa Tanzania kupitia Jiopaki pekee iliyoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Ngorongoro-Lengai, ambayo inatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imekabidhiwa Urais wa mtandao huo katika kikao cha 10 cha Kidunia cha UNESCO Jiopaki kinachofanyika katika mji wa Marrakesh nchini Morocco.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhandisi Joshua Mwankunda (kushoto) akikabidhiwa cheti cha kuwa Rais wa Mtandao wa Jiopaki Barani Afrika kutoka kwa Rais anayemaliza muda wake, Bw.Driss Achbal kutoka nchini Morocco katika vikao vinavyoendelea nchini Morocco kuanzia Septemba 9, 2023
Rais Mpya wa Mtandao wa Jiopaki Afrika aliyechaguliwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mhandisi Joshua Moshi Mwankunda ambaye ni Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni na Jiolojia NCAA.
Rais Mpya wa Mtandao wa Jiopaki Afrika aliyechaguliwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mhandisi Joshua Moshi Mwankunda ambaye ni Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni na Jiolojia NCAA.

1. Kuongezeka kwa muonekano chanya wa nchi ya Tanzania kimataifa,
2. Kuongezeka kwa idadi ya watalii na watafiti watakaotembelea nchi ya Tanzania kwa Shughuli mbalimbali.
3. Kupanua wigo wa mashirikiano ya kimataifa katika sekta ya uhifadhi na utalii wa jiopaki na miamba (Geopark)
4. Fursa ya kuongeza vivutio vingi vya utalii wa miamba kupitia uanzishwaji wa jioapaki mpya nchini Tanzania.